Luke 24

Kufufuka Kwa Isa

(Mathayo 28:1-10; Marko 16:1-8; Yohana 20:1-10)

1 aMnamo siku ya kwanza ya juma, alfajiri na mapema, wale wanawake walichukua yale manukato waliyokuwa wameyaandaa, wakaenda kaburini. 2 bWakakuta lile jiwe limevingirishwa kutoka kwenye kaburi, 3 clakini walipoingia ndani, hawakuuona mwili wa Bwana Isa. 4 dWalipokuwa wanashangaa juu ya jambo hili, ghafula watu wawili waliokuwa wamevaa mavazi yanayong’aa kama umeme wakasimama karibu nao. 5Wale wanawake, wakiwa na hofu, wakainamisha nyuso zao mpaka chini. Lakini wale watu wakawaambia, “Kwa nini mnamtafuta aliye hai miongoni mwa wafu? 6 eHayuko hapa; amefufuka! Kumbukeni alivyowaambia alipokuwa bado yuko pamoja nanyi huko Galilaya kwamba: 7 f‘Ilikuwa lazima Mwana wa Adamu atiwe mikononi mwa watu wenye dhambi na waovu ili asulubiwe, na siku ya tatu afufuke.’ ” 8 gNdipo wakayakumbuka maneno ya Isa.

9 hWaliporudi kutoka huko kaburini, wakawaeleza wale wanafunzi kumi na mmoja pamoja na wengine wote mambo haya yote. 10 iBasi Maria Magdalene, Yoana, na Maria mama yake Yakobo, pamoja na wanawake wengine waliofuatana nao ndio waliwaelezea mitume habari hizi. 11 jLakini hawakuwasadiki hao wanawake, kwa sababu maneno yao yalionekana kama upuzi. 12 kHata hivyo, Petro akainuka na kukimbia kwenda kule kaburini. Alipoinama kuchungulia, akaona vile vitambaa vya kitani, ila hakuona kitu kingine. Naye akaenda zake akijiuliza nini kilichotokea.

Njiani Kwenda Emau

(Marko 16:12-13)

13 lIkawa siku iyo hiyo, wanafunzi wawili wa Isa walikuwa njiani wakienda kijiji kilichoitwa Emau, yapata maili saba
Maili saba ni kama kilomita 11.2.
kutoka Yerusalemu.
14Walikuwa wakizungumza wao kwa wao kuhusu mambo yote yaliyotukia. 15 nWalipokuwa wakizungumza na kujadiliana, Isa mwenyewe akaja akatembea pamoja nao, 16 olakini macho yao yakazuiliwa ili wasimtambue.

17Akawauliza, “Ni mambo gani haya mnayozungumza wakati mnatembea?”

Wakasimama, nyuso zao zikionyesha huzuni.
18 pMmoja wao, aliyeitwa Kleopa, akamuuliza, “Je, wewe ndiye peke yako mgeni huku Yerusalemu ambaye hufahamu mambo yaliyotukia humo siku hizi?”

19 qAkawauliza, “Mambo gani?”

Wakamjibu, “Mambo ya Isa Al-Nasiri. Yeye alikuwa nabii, mwenye uwezo mkuu katika maneno yake na matendo yake, mbele za Mungu na mbele ya wanadamu wote.
20 rViongozi wa makuhani na viongozi wetu walimtoa ahukumiwe kufa, nao wakamsulubisha. 21 sLakini tulikuwa tumetegemea kwamba yeye ndiye angelikomboa Israeli. Zaidi ya hayo, leo ni siku ya tatu tangu mambo haya yatokee. 22 tIsitoshe, baadhi ya wanawake katika kundi letu wametushtusha. Walikwenda kaburini leo alfajiri, 23lakini hawakuukuta mwili wake. Walirudi wakasema wameona maono ya malaika ambao waliwaambia kwamba Isa yu hai. 24 uKisha baadhi ya wenzetu walikwenda kaburini wakalikuta kama vile wale wanawake walivyokuwa wamesema, lakini yeye hawakumwona.”

25Isa akawaambia, “Ninyi ni wajinga kiasi gani, nanyi ni wazito mioyoni mwenu kuamini mambo yote yaliyonenwa na manabii! 26 vJe, haikumpasa Al-Masihi
Al-Masihi maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.
kuteswa kwa njia hiyo na kisha aingie katika utukufu wake?”
27 xNaye akianzia na Torati ya Musa na Manabii wote, akawafafanulia jinsi Maandiko yalivyosema kumhusu yeye.

28 yNao walipokaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, Isa akawa kama anaendelea mbele. 29 zLakini wao wakamsihi sana akae nao, wakisema, “Kaa hapa nasi, kwa maana sasa ni jioni na usiku unaingia.” Basi akaingia ndani kukaa nao.

30 aaAlipokuwa mezani pamoja nao, akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akaanza kuwagawia. 31 abNdipo macho yao yakafumbuliwa, nao wakamtambua, naye akatoweka machoni pao. Hawakumwona tena. 32 acWakaulizana wao kwa wao, “Je, mioyo yetu haikuwakawaka kwa furaha ndani yetu alipokuwa anazungumza nasi njiani na kutufafanulia Maandiko?”

33Wakaondoka mara, wakarudi Yerusalemu. Wakawakuta wale wanafunzi kumi na mmoja na wale waliokuwa pamoja nao, wamekusanyika 34 adwakisema, “Ni kweli! Bwana amefufuka, naye amemtokea Simoni.” 35 aeKisha wale wanafunzi wawili wakaeleza yaliyotukia njiani na jinsi walivyomtambua Isa alipoumega mkate.

Isa Awatokea Wanafunzi Wake

(Mathayo 28:16-20; Marko 16:14-18; Yohana 20:19-23; Matendo 1:6-8)

36 afWalipokuwa bado wanazungumza hayo, Isa mwenyewe akasimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi!”

37 agWakashtuka na kuogopa wakidhani kwamba wameona mzuka. 38Lakini Isa akawauliza, “Kwa nini mnaogopa? Kwa nini mna shaka mioyoni mwenu? 39 ahTazameni mikono yangu na miguu yangu, mwone kuwa ni mimi hasa. Niguseni mwone; kwa maana mzuka hauna nyama na mifupa, kama mnionavyo kuwa navyo.”

40Aliposema haya, akawaonyesha mikono na miguu yake. 41 aiWakashindwa kuamini kwa ajili ya furaha na mshangao waliokuwa nao. Akawauliza, “Mna chakula chochote hapa?”

42Wakampa kipande cha samaki aliyeokwa, 43 ajnaye akakichukua na kukila mbele yao.

44 akAkawaambia, “Haya ndiyo yale niliyowaambia nilipokuwa bado niko pamoja nanyi, kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu mimi katika Torati ya Musa, Manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.”

45 alNdipo akafungua fahamu zao ili waweze kuyaelewa Maandiko. 46 amAkawaambia, “Haya ndiyo yaliyoandikwa: Al-Masihi atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka kwa wafu. 47 anToba na msamaha wa dhambi zitatangaziwa mataifa yote kupitia jina lake kuanzia Yerusalemu. 48 aoNinyi ni mashahidi wa mambo haya.

Kuahidiwa Kwa Roho Mtakatifu

49 ap“Tazama nitawatumia ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini hadi mtakapovikwa uwezo utokao juu.”

Kupaa Kwa Isa Mbinguni

(Marko 16:19-20; Matendo 1:9-11)

50 aqAkiisha kuwaongoza mpaka kwenye viunga vya Bethania, akainua mikono yake juu na kuwabariki. 51 arAlipokuwa anawabariki, akawaacha, akachukuliwa mbinguni. 52 asKisha wakamwabudu na kurudi Yerusalemu wakiwa wamejawa na furaha kuu. 53 atNao wakadumu ndani ya Hekalu wakimtukuza Mungu. Amen.
Copyright information for SwhKC